The Hague. Kamanda ahukumiwa kwenda jela miaka 26.
4 Novemba 2006Matangazo
Mahakama ya kuwahukumu wahalifu wa vita nchini Bosnia imemhukumu kamanda mmoja wa wakati wa vita Mserbia kwenda jela miaka 26.
Marko samardzija , mwenye umri wa miaka 70 alikutikana na hatia ya kuamuru mauaji ya Waisamu 144 wakati wa vita vya Bosnia mwaka 1992-95.
Mahakama hiyo pia imemhukumu Mserb mwingine, Nikola Kovacevic , kwenda jela miaka 12 kwa uhalifu wa kivita dhidi ya Waislamu na Wakroati katika jimbo la jirani la Sanski.