Tarehe za Kombe la Dunia Qatar 2022 zachaguliwa | Michezo | DW | 21.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Tarehe za Kombe la Dunia Qatar 2022 zachaguliwa

Shirikisho la Kandanda la Kimataifa - FIFA, limeamua fainali ya mashindano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar itachezwa mnamo Desemba 18. Hii ni kuepuka kiwango cha joto kali nchini humo

Msemaji wa FIFA Walter de Gregorio alitangaza taarifa hiyo mjini Zurich mnamo siku ya Alhamisi. Kamati tendaji ya Shirikisho hilo ilikuwa na kikao kimoja tu na kuchukuwa uamuzi huo kuyabadilisha mashindano hayo kutoka mwezi Juni hadi Julai na kuwa katika tarehe za Novemba hadi Desemba .

Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Kombe la dunia tangu 1930, kwa mashindano ya kombe la dunia wakati Ulaya ukiwa ni msimu wa baridi, kwa sababu msimu wa joto Ulaya ni wa joto kali kabisa huko Qatar na hivyo hali ya hewa itazusha matatizo kwa mashabiki kutoka kwengineko duniani

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, rtre, afp
Mhariri: Saumu Yusuf

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com