1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tani 2.7 za madawa ya kulevya zakamatwa kwenye ndizi

Mohammed Khelef
17 Mei 2023

Polisi wa Italia wamekamata tani 2.7 za madawa ya kulevya aina ya kokeni yaliyokuwa yamefichwa ndani ya shehena ya ndizi.

https://p.dw.com/p/4RUJG
Großeinsatz gegen Mafia in Europa | Italien San Luca
Picha: ROPI/picture alliance

Madawa hayo ya kulevya yanayokisiwa kuwa na thamani ya takribani Euro milioni 800 yalikamatwa na polisi katika eneo la Calabria, ambalo ni makao makuu ya magenge ya uhalifu barani Ulaya.

Makontena ya shehena hiyo ya mihadharari ilikuwa inaelekea Georgia.

Madawa hayo ya kulevya yaligunduliwa kutokana na kamera maalumu na mbwa waliofundishwa kuitambuwa mihadharati kwa kunusa.

Soma zaidi: Kesi kubwa dhidi ya Mafia kuanza Italia

Polisi ya Italia imesema kukamatwa kwa madawa hayo ni hatua muhimu katika kazi za polisi za kupambana na wahalifu sugu wa kundi la Ndrangheta kwenye eneo la Calabria.

Kundi hilo pia linaendesha shughuli zake za kihalifu katika nchi za Ujerumani, Uholanzi na katika nchi za Ulaya ya Mashariki.