1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban wapiganaji 200 wauawa kwenye machafuko mapya Yemen

4 Januari 2022

Takriban wapiganaji 200 wameuawa kufuatia mapigano mapya yaliyozuka katika mji wa kimkakati wa Marib nchini Yemen. Saumu Njama na maelezo zaidi.

https://p.dw.com/p/458Ls
Jemen | Kämpfe in Marib
Picha: AFPTV/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa duru za kitabibu zaidi ya waasi 125 wa Kihouthi wameuawa kufuatia mashambulizi ya ndege yaliyofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, wakati makabiliano yalipotokea kati ya waasi na vikosi vya serikali, katika majimbo ya Shabwa na Al-Bayda. soma Muungano wa kijeshi wadai kuwauwa waasi 165 Yemen

Haya yanajiri wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen ambavyo vimedumu kwa miaka saba nchini humo vikiendelewa kuongezeka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya serikali ya muungano wa kijeshi unaaongwa mkono serikali ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, umepoteza wanajeshi wake 70 katika mapigano hayo yalifanyika katika muda wa saa 24 zilizopita.

soma Zaidi ya waasi 150 wa Yemen wauawa katika mashambulizi Yemen

Mamilioni ya watu wamelazimika kuyakimbia makaazi yao kufuatia machafuko ya Yemen ambayo pia yamesababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unataja kuwa mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu.

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umekuwa ukipigana kwa takriban miaka saba kuunga mkono serikali ya Yemen dhidi ya Wahuthi, katika mzozo ambao umesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao na kusababisha mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. 

soma Hali ya Kiutu yazidi kuwa mbaya nchini Yemen

Serikali itachukua hatua 

Jemen | Kämpfer gegen die Huthi-Rebellen nahe Marib
Picha: Nariman El-Mofty/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia Turki al-Maliki amesema: "Tutachukua hatua zote dhidi ya wanamgambo wa Huthi. Raia wa Saudia na wakaazi wa wake ni mstari mwekundu, na wanamgambo wanapaswa kufikiria mara elfu moja na kutokata tamaa kwa udikteta wa Walinzi wa Mapinduzi wa Iran uliopo Sanaa. Tutachukua hatua zote kuharibu uwezo huo kama tulivyofanya kwenye operesheni yetu wiki jana. Tutachukua hatua kali na kuzindua mashambulizi makali dhidi ya wanamgambo wa Huthi iwapo watawalenga raia."

Huku uhasama ukiongezeka, waasi wa Kihouthi jana Jumatatu walisema wamekamata meli ya kijeshi iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Muungano huo ulisisitiza kuwa ulikuwa umebeba vifaa vya matibabu.

Mwezi Septemba, waasi walizidisha juhudi zao za kutaka kuudhibiti mji mkuu wa mkoa Marib, ambao ni ngome ya mwisho ya serikali kaskazini mwa nchi.

Katika wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la mashambulizi ya anga kutoka Saudia dhidi ya maeneo ya waasi wa Kihouthi, na waasi hao wakijibu kwa kuongeza mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kwenye ufalme huo wa kiarabu.

Kulingana na matabibu wa Medecins Sans Frontieres  siku ya jumapili pekee takriban majeruhi thelathini na tisa walifika katika hospitali ya Ataq iliyoko Shabwa.

 

Chanzo: AFP