1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Taiwan yakosoa uchokozi wa China kufuatia luteka za kijeshi

24 Mei 2024

Siku tatu baada ya kuapiswa kwa Rais mpya wa Taiwan, China imeanza luteka za kijeshi yanayoonekana kuonesha hali halisi ya mzingiro wa kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4gDYO
Taiwan | Huang Wen-chi naibu mkuu wa upelelezi | Mkutano na waandishi wa habari Wizara ya Ulinzi
Huang Wen-chi naibu mkuu wa upelelezi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Taipei.Picha: Annabelle Chih/REUTERS

Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema pia kuwa iligundua meli za kijeshi za China zisizopungua 15, meli 16 za kikosi cha ulinzi wa pwani na zaidi ya ndege 40 za kivita karibu na kisiwa hicho.

Zaidi ya ndege 35 za jeshi la China zilionekana zikivuka msitari unaogawa ujia wa bahari wa Taiwan.

Meja Jenerali Wu I-Sheng, aliuambia mkutano wa habari jana jioni, kwmaba hatua za China zimekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kitisho au matumizi ya nguvu dhidi ya mamlaka ya mipaka au uhuru wa kisiasa wa taifa jengine.

Luteka hizo zinatarajiwa kumalizika leo Ijumaa na huenda zikawa ndiyo kubwa zaidi katika kipindi cha karibu mwaka mmoja.