1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak na Starmer washiriki mdahalo wa kwnaza wa televisheni

5 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na kiongozi wa upinzani wa chama cha Labour Keir Starmer jana wamekabiliana katika mdahalo wa televisheni kuhusu jinsi ya kuuinua uchumi wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4gexk
Uingereza |Kampeni za uchaguzi uchaguzi mkuu |Rishi Sunak
Rishi Sunak Waziri Mkuu wa Uingereza na kiongozi wa Chama cha Conservative Rishi SunakPicha: Henry Nicholls/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu Sunak amekilaumu chama cha Labour akisema kinataka kuongeza kodi iwapo kitashinda uchaguzi wa Julai 4. Katika mdahalo wao wa kwanza, viongozi wote wawili walionekana kujipigia debe huku zikiwa zimesalai wiki chache tu kabla Waingereza hawajapiga kura katika uchaguzi mkuu. Sunak amesema kwamba yeye ndiye aliye na mpango wa kuukuzauchumi wa Uingereza ambao unakuwa kwa kasi ndogo huku Starmer akidai kwamba uchumi wa Uingereza umekuwa katika mtafaruku mkubwa kutokana na usimamizi wa miaka 14 wa chama cha Kihafidhina. Viongozi hao pia wameelezea hoja zao kuhusiana na jinsi watakavyokabiliana na mzozo wa gharama ya maisha, afya ya umma na kuuboresha mfumo wa elimu nchini humo.