Sudan yawafukuza maafisa wawili wa Shirika la WFP
29 Oktoba 2025
Matangazo
Serikali ya Sudan imesema jana kuwa wawili hao wamepewa muda wa saa 72 kuondoka nchini humo.
Hata hivyo haikutoa sababu za uamuzi huo.
Hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Sudan kuchukua hatua kama hiyo dhidi ya Umoja wa Mataifa.
Sio mara ya kwanza kwa Sudan kuwafukuza wafanyakazi wa UN
Mnamo Juni 2023, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes, alitangazwa kuwa mtu asiyestahili kuwa nchini humo.
Alituhumiwa wa kuchochea vita nchini humo, ambavyo vimedumu sasa kwa zaidi ya miaka miwili.
Siku ya Jumatatu, jeshi la Sudan lilitangaza kujiondoa kutoka El Fashir, mji muhimu katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan, na kuuacha chini ya udhibiti wa kikosi cha wanamgambo cha RSF.