1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Stoltenberg: Ukraine na washirika "wasikate tamaa"

Lilian Mtono
24 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ametoa wito kwa Ukraine na washirika wake kutokata tamaa wakati Rais wa Urusi akiendeleza mashambulizi makali katika vita hivyo vinavyoingia mwaka wa tatu.

https://p.dw.com/p/4cpVM
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ametoa wito kwa Ukraine na washirika wake kutokata tamaa wakati Rais wa Urus
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ametoa wito kwa Ukraine na washirika wake kutokata tamaa wakati Rais wa UrusPicha: Kuhlmann/MSC

Stoltenberg amesema katika ujumbe uliorekodiwa wa kumbukumbu ya miaka miwili ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kuwa hali kwenye uwanja wa mapambano bado ni mbaya sana.

Amesema lengo la Rais Putin kuidhibiti Ukraine halijabadilika na hakuna ishara kuwa anajiandaa kwa mpango wa amani. Ameipongeza Ukraine kwa kuonyesha ustadi mkubwa na dhamira ya kweli ya kupambana tena na tena.

Wanajeshi wa Ukraine wasiokuwa na silaha za kutosha wanajitahidi kupambana kwenye uwanja wa vita wakati kukiwa na mashaka kuhusu uungaji mkono wa Marekani katika siku za usoni.