1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yamesababisha vifo vya watu 50 Somalia.

21 Novemba 2023

Watu wasiopungua 50 wamekufa na wengine karibu 700,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mafuriko nchini Somalia

https://p.dw.com/p/4ZFaM
Somalia Mogadischu | Überschwemmungen nach Starkregen
Picha: Feisal Omar/REUTERS

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na afisa wa serikali ya Mogadishu ambaye ameonya kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi. Mkurugenzi wa Shirika la Kudhibiti Maafa la Somalia Mohamud Moalim Abdullahi amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba mvua zinazotarajiwa kunyesha kati ya tarehe 21 na 24 Novemba, zinaweza kusababisha mafuriko zaidi ambayo yatapelekea pia vifo na uharibifu mkubwa.Shirika la misaada la Uingereza la "Save the Children" limesema wiki iliyopita kuwa zaidi ya watu 100, wakiwemo watoto 16, wamefariki dunia katika nchi za Kenya, Somalia na Ethiopia kutokana na mafuriko. Eneo la Pembe ya Afrika linakabiliwa na mvua kubwa pamoja na mafuriko yanayohusishwa na matokeo ya hali ya hewa ya El Nino.