Sissi aapishwa kwa muhula wa tatu Misri
2 Aprili 2024Al- Sissi mwenye umri wa miaka 69 na ambaye ameliongoza taifa hilo kwa zaidi ya muongo mmoja, ataanza rasmi muhula wake mpya hapo kesho, ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu baada ya kuchaguliwa tena kama rais wa nchi hiyo kwa asilimia 89.6 za kura.
Mustafa Bakri, mbunge mwenye ushirikiano wa karibu na mamlaka nchini humo, amesema kulingana na katiba, muhula huu mpya wa miaka sita, unatarajiwa kuwa wa mwisho kwa uongozi wa Sissi.
Soma zaidi: Wamisri wanapiga kura leo kumchagua Rais
Mbunge huyo aliongeza kuwa huenda serikali ikajiuzulu baada ya kuapishwa kwaSissi kuruhusu kufanyika mabadiliko katika baraza la mawaziri.
Kuapishwa kwa Sissi kunakuja wakati ambapo taifa hilo linakabiliwa na mzozo mbaya wa kiuchumi, kuongezeka kwa mfumuko wa bei na uhaba wa sarafu za kigeni.
Lakini mwanzoni mwa mwaka huu, Misri ilipokea mikopo kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).