Shirika la Msalaba Mwekundu: Upotoshaji unahujumu misaada
5 Machi 2026
Matangazo
Katika ripoti yake ya Majanga ya Dunia kwa mwaka 2026,shirika hilo la Msalaba Mwekundu limesema kati ya mwaka 2020 na 2024, majanga yaliwaathiri zaidi ya watu milioni 700 ambapo milioni 105 waliyahama makaazi yao na takriban watu 270,000 wakaaga dunia.
Idadi ya watu waliohitaji misaada ya kiutu katika kipindi hicho hicho, iliongezeka mara dufu. Lakini shirika hilo limeongeza kuwa, taarifa za kupotosha ni jambo linalozidi kuhujumu imani, na kuyaweka maisha ya wafanyakazi wa kutoa misaada ya kiutu hatarini.
Shirika la Msalaba Mwekundu lina zaidi ya wafanyakazi milioni 17 wa kujitolea katika zaidi ya nchi 191 kote duniani.