1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Mamlaka ya Palestina yatangaza baraza jipya la mawaziri

28 Machi 2024

Mamlaka ya Palestina imetangaza baraza jipya la mawaziri katikati ya shinikizo la kimataifa la kufanya mabadiliko. Rais Mahmoud Abbas ameitangaza serikali hiyo mpya kutokana na amri ya rais.

https://p.dw.com/p/4eEHc
Palestina-Rais Mahmoud Abbas
Rais wa Palestina Mahmud Abbas akionekana wakati wa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), huko Riyadh, Saudi Arabia Novemba 11, 2023, kushiriki mkutano wa kilele.Picha: Saudi Press Agency/Newscom/picture alliance

Mawaziri wote aliowataja hawana umaarufu mkubwa. Karibu watano kati ya mawaziri 23 wanaoingia serikalini wanatokea Gaza ingawa haijajulikana iwapo bado wapo katika eneo hilo.

Tafiti za maoni za miaka ya hivi karibuni zimeonesha kwamba Wapalestina walio wengi wanamtaka Abbas mwenye umri wa miaka 88 aachie ngazi.

Mamlaka ya Palestina inasimamia sehemu ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Waisraeli na haina mamlaka Gaza baada ya majeshi yake kufukuzwa baada ya kundi la Hamas kuchukua madaraka mwaka 2007.

Wapalestina wachache ndio wanaoiunga mkono mamlaka hiyona hasa kwa sababu ya kutofanyika uchaguzi katika kipindi cha miaka 18.