1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz afanya ziara ya siku mbili Mashariki ya Kati

16 Machi 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anaelekea Israel na Jordan leo Jumamosi kwa ziara ya siku mbili ya Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4dngz
Berlin | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa kwenye mkutano wa pamoja na kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa kwenye mkutano wa pamoja na kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud AbbasPicha: Wolfgang Kumm/dpa/picture alliance

Msemaji wa serikali Steffen Hebestreit ameeleza kuwa kiongozi huyo wa Ujerumani kwanza ataizuru Jordan alafu baadaye ataelekea Israel.

Mkutano kati ya Scholz na Mfalme Abdullah II wa Jordan umepangwa kufanyika kwanza halafu kesho Jumapili, Scholz ataelekea Israel ambako amepangiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Soma pia: Mkutano wa Scholz na Biden, kipi kitarajiwe? 

Kansela huyo wa Ujerumani pia atakutana na Rais wa Israel Isaac Herzog. Hata hivyo, halimo kwenye mipango yake swala la kukutana na wawakilishi wa Mamlaka ya Palestina.

Hii ni ziara ya pili ya Scholz katika eneo hilo la Mashariki ya Kati tangu shambulio la wanamgambo wa Hamas la Oktoba 7 mwaka uliopita.