1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudia yashambulia bandari ya Yemen juu ya silaha kutoka UAE

30 Desemba 2025

Saudi Arabia leo imeshambulia kwa mabomu mji wa bandari wa Mukalla nchini Yemen, sehemu inayoelezwa kuhifadhi shehena ya silaha za kikosi cha wanajeshi waliojitenga iliyowasili kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE.

https://p.dw.com/p/567DY
Yemen Mukalla 2025 | Shambulizi la mabomu
Uharibifu uliofanywa na shambulizi la Saudi Srabiakatika bandari ya Mukalla nchini Yemen mnamo Desemba 30, 2025Picha: Murad/Xinhua News Agency/picture alliance

Pia Saudia iliuhusisha moja kwa moja Umoja huo wa Falme za Kiarabu kwa mashambulizi ya hivi karibuni ya kikosi hicho huko Yemen na kuuonya kuwa vitendo vyake ni "hatari sana," na kuitaka UAE kujiondoa nchini Yemen.

Baadaye, vikosi vya Yemen vinavyolipinga kundi la Wahouthi, vilitangaza hali ya hatari na kusitisha ushirikiano wake na UAE huku vikiamuru vikosi vyote vya Umoja huo ndani ya ardhi yake kuondoka ndani ya masaa 24.

Pia vilitoa marufuku ya masaa 72 ya kutumia vivuko vyote vya mpaka katika maeneo wanayoshikilia, pamoja na viingilio vya viwanja vya ndege na bandari, isipokuwa vile vilivyoruhusiwa na Saudi Arabia. Hata hivyo UAE haikutoa tamko la haraka kuhusu hali hiyo.