Saudi Arabia, Qatar na Oman yamshawishi Trump kuhusu Iran
15 Januari 2026
Matangazo
Afisa huyo aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema mataifa hayo matatu ya Ghuba yaliongoza juhudi pana za kidiplomasia za dakika za mwisho kumshawishi Trump kuipa Iran nafasi ya kuonyesha nia njema.
Amesema mazungumzo bado yanaendelea kudumisha imani iliyoko.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, limesema kwamba afisa mmoja wa Shirika lake la Hilali Nyekundu Amir Ali Latifi ameuawa na wenzake wengine watano kujeruhiwa walipokuwa kazini mkoani Gilan kaskazini-magharibi mwa Iran mnamo Januari 10.
Haya ni kulingana na maelezo kupitia taarifa yake iliyotoa kutoka makao yake makuu huko Geneva, bila kutoa maelezo zaidi.