1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia kutumia uwekezaji wa mabilioni ya dola kisiasa?

Zainab Aziz
4 Oktoba 2022

Saudi Arabia inatumia utajiri wake wa mafuta kuwekeza pakubwa katika mataifa mengine, ikijaribu kubadili uchumi wake. Wakosoaji wanahofia kwamba nguvu yote hiyo ya kifedha nje inaweza kutumiwa kwa malengo ya kisiasa.

https://p.dw.com/p/4Hje3
Bin Salman mit Olaf Scholz in Jeddah
Picha: Balkis Press/abaca/picture alliance

Kumekuwepo miito ya mara kwa mara ya kuisusia Saudi Arabia kwa sababu ya kuhusishwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu. Lakini yeyote anayejaribu kuchukua hatua ya kuitenga Saudi Arabia basi atakuwa kwenye wakati mgumu kwani kufanya hivyo ni sawa na kuzuia uwekezaji mkubwa wa nchi hiyo katika taifa husika.

Katika miaka sita iliyopita, uwekezaji wa Saudi Arabia kimataifa umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Hazina ya utajiri wa Saudi Arabia inayomilikiwa na serikali sasa ina hisa katika kampuni kubwa kubwa duniani kama Amazon, Google, Visa, Microsoft, Disney, Nintendo, Uber, PayPal na Zoom.

Soma pia: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko Saudi Arabia kusaka nishati kwenye nchi za Ghuba

Zingine ni kampuni inayoandaa likizo za kitajiri - Carnival, Saudi Arabia inamiliki pia timu ya soka ya Ligi Kuu ya Uingereza, Newcastle United na vilevile Saudi Arabia ina uhusiano mkubwa na kampuni ya BlackRock, msimaizi mkuu wa mali duniani na kampuni zingine nyingi.

Russische Desinformation im Nahen Osten | MBS und Putin in Osaka
Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman akiwa na Rais wa Urusi Vladmir Putin wakati wa Mkutano wa Kilele wa G20 nchini Japan, Juni 29,2019.Picha: Yuri Kadobnov/AFP/AP/picture alliance

Mabadiliko makubwa

Kwa hakika, kila wakati unaponunua kahawa katika mkahawa wa Starbucks, au unapocheza mchezo wa mtandaoni wa World of Warcraft, moja kwa moja unaunga mkono uwekezaji wa Saudi Arabia.

Sababu ya nchi hiyo kuwa na hisa katika kampuni zenye majina ni Hazina yake ya Uwekezaji wa Umma, PIF.  PIF ilianzishwa nchini humo mnamo mwaka 1971 lakini hadi hivi majuzi, mfuko huo wa Saudi Arabia ulifanya uwekezaji wa chini ndani ya nchi na hata kimataifa.

Soma pia: Biden atarajia mafuta zaidi na ujumuishwaji wa Israel Arabuni

Lakini yote yalibadilika mnamo mwaka 2015 wakati mtawala wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, ambaye mara nyingi huitwa MBS, alipoanza kuunganisha utajiri wa ufalme huo kwa jina lake.

MBS aliifanya PIF kuwa kitovu cha mipango yake ya kuifanya Saudi Arabia kuwa nchi ya kisasa na kuutofautisha uchumi wake na utajiri wa mafuta.

Mnamo mwaka wa 2016, mfuko huo uligonga vichwa vya habari duniani kwa kuwekeza dola bilioni 3.5 katika kampuni ya usafiri ya Uber.

Saudi-Arabien Besuch Präsident Erdogan bei Mohammed bin Salman
Mohammed bin Salman akikutana na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, mjini Jeddah, Aprili 28, 2022.Picha: MURAT C. MUHURDAR/Turkish Presidency/AFP

Hata hivyo kadiri mfuko wa PIF nchini Saudi Arabia, na kiongozi mwenye mamlaka aliye nyuma ya uwekezaji mkubwa wa nchi hiyo kimataifa wanavyozidi kuwa na nguvu duniani, baadhi ya wadadisi na wachambuzi wameeleza wasiwasi na kuuliza maswali Je, uwekezaji wote huo wa kimataifa ni sawa na nguvu za kisiasa?

Soma pia: Mwanamfalme bin Salman aizuru Uturuki

Na Je, Saudi Arabia inatumia mfuko wake wa PIF wa uwekezaji kimataifa kujijengea ushawishi kutimiza malengo ya sera yake ya kigeni?

Jukumu lisilokifani

Karen Young, mtafiti mkuu katika kitengo cha sera za nishati ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Columbia, amebainisha kuwa jukumu jipya la PIF katika uchumi wa Saudi Arabia halina kifani.

Mauaji ya Khashoggi: Trump aweka pesa mbele ya haki za binadamu

Soma pia: Uturuki, Saudia zaahidi ushirikiano wa karibu baada ya mvutano wa Khashoggi

Young, ambaye sasa anaandaa kitabu kuhusu fedha za utajiri huru katika mataifa ya Ghuba, ameiambia DW kuwa mataifa Tajiri ya Ghuba yamekuwa yanalenga kuwekeza nchini Ugiriki kwa sababu za kiulinzi na nchini Ujerumani yanalenga kufanikisha mikataba ya nishati.

Sara Bazoobandi, mshirika katika Taasisi ya GIGA inayotoa Mafunzo kuhusu Mashariki ya Kati yenye makao yake mjini Hamburg amesema cha muhimu kutambua kwamba motisha moja wapo ya kawaida ya uwekezaji wa fedha ni kuongeza mapato ya kifedha na kwamba Wasaudi, angalau hawajali sana juu ya ushawishi wao kisiasa bali wanachojali zaidi ni kutumia nafasi yao kupata faida zaidi.

Chanzo: DW