1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sasa 300 ndio wameuawa Kenya

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjTX

NAIROBI.

Idadi ya waliouliwa katika ghasia zilizofuatia uchaguzi wa mwishoni mwa Juma nchini Kenya inaongezeka kupanda.

Kwa mujibu wa shirika lisililo la kiserikali linalotetea haki za binadamu la nchini Kenya-la- Kenya Human Rights Commission-KHRC-sasa idadi haipungui 300.

Na mamia ya wengi wametoroka makwao wakikimbia ghasia. Wengine wamekimbilia hifadhi katika nchi jirani kama vile Uganda.

Juhudi za kikanda zinachukuliwa ili kupatanisha pande mbili husika-Rais Mwai Kibaki na mpinzani wake -Raila Odinga. Nayo jamii ya kimataifa imetoa mwito wa kukomesha ghasia.

Matukio mbalimbali ya ghasia yametokea nchini humo tangu disemba 27 mwaka uliopita.

Na katika tukio moja baya zaidi, watu wasiopungua 30 walichomwa hadi kufa wakiwa ndani ya kanisa moja katika eneo la Eldoret.Watu wapatao 100 walikuwa wamekimbilia mahali hapo wakitoroka ghasia.

Kibaki na mpinzani wake wa kisiasa,Raila Odinga wanalaumiana kwa kuwa chanzo cha ghasia hizo.Odinga anasema matokeo yaligangwa.Yeye mkuu wa tume ya uchaguzi ya Kenya-Samuel Kivuitu asema hajafanya makosa yoyote kwani alitangaza yale aliokuwa akipata kutoka mikoani.

Chama cha ODM cha Raila Odinga kinapanga mkutano mkuu mjini Nairobi alhamisi licha ya serikali kuukataa.Alexander Graf Lambsdorff ni mkuu wa tume ya wachunguzi wa uchaguzi wa Kenya kutoka Ulaya.Katika mahojiano na DW amegusia suala hilo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-John Kufuor anajaribu kupatanisha pande mbili husika ili kukomesha ghasia.