1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki sawaAfghanistan

Saluni, maduka ya urembo yafungwa leo Afghanistan

Tatu Karema
25 Julai 2023

Maelfu ya maduka ya urembo kote nchini Afghanistan leo yanatarajiwa kufungwa kabisa kufuatia agizo la serikali ya Taliban la kufunga mojawapo ya njia chache za mapato kwa wanawake pamoja na nafasi nzuri ya kujumuika.

https://p.dw.com/p/4ULKz
Schönheitssalons in Afghanistan verboten
Picha: ALI KHARA/REUTERS

Mwishoni mwa mwezi Juni, Wizara ya Kuamrisha Mema na Kuzuia Maovu ilitoa muda wa mwisho wa hadi leo kwa saluni zote kufungwa na kusema muda huo ungewezesha wafanyabiashara hao kumaliza matumizi ya bidhaa zilizobakia.

Wizara hiyo imesema ilitoa agizo hilo kwa sababu pesa nyingi zinazotumika kwa urembo zinasababishia hali ngumu kwa familia maskinina kwamba baadhi ya huduma katika saluni hizo haziendani na maadili ya Kiislamu.

Soma pia:Mkuu wa jeshi la Pakistan auonya utawala wa Taliban dhidi ya kuhifadhi makundi ya kigaidi

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa vipodozi vingi vinawazuia wanawake kutawadha vizuri kwa ajili ya sala huku kuongeza kope na kusuka nywele pia kukipigwa marufuku.

Nakala iliyoonekana na shirika la habari la AFP, inasema maagizo hayo ya mdomo yanatoka kwa kiongozi mkuu, Hibatullah Akhundzada.