1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rubio apigia debe nishati ya Marekani nchini India

23 Mei 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amekutana leo na waziri mkuu wa India Narendra Modi na kujadili kuhusu biashara na nishati, katika ziara inayolenga kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/5EEVf
India, New -Delhi 2026 | Narendra Modi na Marco Rubio wafanya mazungumzo Mei 23, 2026
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio ( kushoto) na waziri mkuu wa India Narendra Modi (kulia)Picha: ANI News/IMAGO

Afisi ya Rubio, imesema amesisitiza kuwa Marekani haitairuhusu Iran kushikilia mateka soko la nishati la dunia.

Mgogoro wa nishati uliosababishwa na vita vya Iran umerudisha nyuma juhudi za Marekani za kuondoa utegemezi wa India kwa mafuta ya Urusi.

Wakati huo huo,  Modi akikosa kuitaja moja kwa moja Iran katika mkutano huo wa leo, alisisitiza uungaji mkono wa India kwa juhudi za amani na akatoa wito wa utatuzi wa migogoro wa amani kwa njia ya mazungumzo na diplomasia. Haya ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya India.

Huku hayo yakijiri, balozi wa Marekani nchini India Sergio Gor, amesema Rubio alitoa mualiko kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump kwa Modi kutembelea ikulu ya White House katika siku zijazo.