1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuKimataifa

Ripoti: Wanaharakati wa mazingira 142 waliuawa 2024

17 Septemba 2025

Wanaharakati wa mazingira wasiopungua 142 waliuawa kote duniani mwaka uliopita na wengine wanne hawajulikani waliko.

https://p.dw.com/p/50aQF
Uchimbaji holela wa madini
Shirika la Global Witness linasema miongoni mwa wanaharakati wanaolengwa ni wale wanapambana dhidi ya uchimbaji haramu wa madini.Picha: Supplied by a Global Witness partner

Hayo ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali la Global Witness. Ripoti hiyo inasema wengi ya waliolengwa walikuwa wakipigania haki za watu wa jamii za asili au wakulima wadogo.

Wengine ni pamoja na wale waliokuwa wanapambana dhidi ya uchimbaji haramu wa madini, biashara ya magogo, ujangili na miradi ya nishati.

Kulingana na ripoti, kwa mara nyingine Colombia imeongoza kwa idadi kubwa ya vifo 48 vya wanaharakati wa mazingira ikifuatiwa na Guatemala, Mexico na Brazil.

Watafiti wamesema mauaji mengi yalifanywa na makundi ya wahalifu na katika baadhi ya matukio vyombo vya usalama wa taifa vilihusika.