Real Madrid bado ni vinara La Liga, Barca waponea | Michezo | DW | 10.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Real Madrid bado ni vinara La Liga, Barca waponea

Barcelona waliponea chupuchupu katika mechi yao ya Jumapili walipokuwa wakichuana na Real Betis ambapo mchuano huo ulishuhudia mabao matano, Barca wakishinda magoli matatu kwa mawili.

Ushindi huo umekuja siku chache baada ya kubwagwa moja bila na Athletic Bilbao na kubanduliwa kwenye kile kikombe cha Copa del Rey. Kocha Quique Setien alikuwa na haya ya kusema.

"Nafikiri tutalazimika kujaribu kushinda kila mechi, ni muhimu sana. Pointi tatu ni muhimu sana kwasababu tunataka kuwa katika mashindano ya kuwania ubingwa wa ligi mpaka dakika ya mwisho," alisema Setien.

Real Madrid walizidisha uongozi wao kwenye ligi hiyo kwa kuwafumania Osasuna nne moja licha ya kuwa Osasuna ndiye aliyekuwa mwenyeji.

Sasa kwa ushindi huo Madrid wanaongoza kwa pointi hamsini na mbili pointi tatu mbele ya Barcelona ambao pointi zao ni arubaini na tisa.

Getafe ni wa tatu wakiwa na pointi arubaini na mbili kisha Atletico Madrid na Sevilla wanafuatana katika nafasi za nne na tano wakiwa na pointi sawa thelathini na tisa kila mmoja.