Rais wa zamani wa Misri Morsi ahukumiwa miaka 20 jela | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.04.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Rais wa zamani wa Misri Morsi ahukumiwa miaka 20 jela

Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa makosa ya kusababisha kuuliwa waandamanaji mwaka 2012.

Rais wa Zamani wa Misri Mohamed Morsi

Rais wa Zamani wa Misri Mohamed Morsi

Korti ya makosa ya jinai mjini Cairo imetoa hukmu hiyo wakati Morsi na watuhumiwa wengine katika kesi hiyo-wengi wao wakiwa viongozi wa chama cha Udugu wa kiislam-wakisimama ndani ya tundu la vigae ndani ya ukumbi wa mahakama katika chuo cha mafunzo ya polisi mjini Cairo.

Kesi yao inahusu matumizi ya nguvu yaliyotokea nje ya kasri la rais mwezi decemba mwaka 2012.Wafuasi wa Morsi waliwashambulia waandamanaji wa upande wa upinzani na kusababisha machafuko yaliyopelekea watu wasiopungua 10 kuuwawa.

Jaji Ahmed Youssouf ameachilia mbali madai ya kuchochea mauaji ya waandamanaji wawili na mwandishi habari mmoja machafuko hayo yaliporipuka mbele ya kasri la rais-madai ambayo wadadisi wengi walikuwa wakifikiriaa yangepeleka Morsi kuhukumiwa adhabu ya kifo.

Morsi na watuhumiwa wenzake wakumbusha yaliyotokea katika msikiti wa Rabaah al Adawiya

Ägypten Muslimbrüder zum Tode verurteilt

Kiongozi wa Udugu wa kiislam,Mohamed Badie,aliyehukumiwa adhabu ya akifo,anapelekwa mahakamani akasikilize hukmu ya wanachama wenzake wa udugu wa kiislam

Mbali na Mohamed Morsi,wakuu wengine 12 wa chama cha Udugu wa kiislamu na wafuasi wa itikadi kali akiwemo Mohammed el Beltagy na Essam el Erian,nao pia kila mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Akitoa hukmu hiyo jaji Ahmed Youssouf ameyataja majina ya mtuhumiwa wote na kufafanua :"Mohammed Mohamed Mursi, Mohammed el Baltagy na Essam el Erian wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa ushiriki wao wa kuchochea mauwaji ya umma wa wamisri na tuhuma za kulidhuru taifa la Misri."

Morsi na watuhumiwa wenzake walinyoosha vidole vinne-alama inayokumbusha malalamiko yaliyofanywa katika msikiti wa Rabaah al Adawiya ambako polisi waliingia kwa nguvu wakawauwa mamia ya waandamanaji wafuasi wa Morsi Agosti 14 mwaka 2013.

Kesi zilisosalia dhidi ya Mursi hazitaharakishwa

Ägypten Mursi Urteil

Hukmu dhidi ya Morsi

Morsi anakabiliwa na kesi nyengine nne pamoja na wanachama wenzake wa udugu wa kiislamu,tangu alipopinduliwa na wanajeshi decemba mwaka 2013.Morsi na wenzake wana nafasi ya kukata rufaa dhidi ya hukmu ya leo.

Wadadisi wanahisi viongozi wa Misri hawatofanya pupa kusikiliza kesi nyengine kwakua hakuna ghasia majiani na wafuasdi wa Udugu wa kiislamu hawakusayiki kwa wingi ili kuepusha wasikamatwe..

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AP/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com