Marais wa China Xi Jinping na wa Urusi Vladimir Putin wametoa kauli zinazoashiria kuimarika kwa uhusiano wao wa kimkakati wakati wa mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika mjini Beijing. Ziara ya Putin ya siku mbili ameifanya siku chache baada ya kumalizika kwa ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini China.