Rais mpya apatikana Somalia. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Rais mpya apatikana Somalia.

Rais mpya wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed ameapishwa kutumikia wadhifa huo.

Rais mpya wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed.

Rais mpya wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed.

DJIBOUTI.

Kiongozi wa kiislamu mwenye mtazamo wa ukadirifu Sheikh Sharif Ahmed ameapishwa kuwa rais mpya wa Somalia baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika mjini Djibouti.

Sheikh Ahmed aligombea katika uchaguzi huo kwa niaba ya chama cha ukombozi wa Somalia -Alliance for Reliberation of Somalia.Alifanikiwa kupata kura nyingi katika raundi ya pili ya uchaguzi baada ya mgombea mwengine mzito, waziri mkuu Nur Hassan Hussein kujitoa.

Uchaguzi huo ulifanyika kufuatia kujiuzulu kwa rais wa hapo awali bwana Abdullahi Yusuf kutokana na mvutano mkubwa baina yake na waziri mkuu Nur Hassan Hussein.Bwana Abdullahi Yusuf alijiuzulu mnamo mwezi desemba mwaka jana.


 • Tarehe 31.01.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GkYn
 • Tarehe 31.01.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GkYn
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com