1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kenyatta aitisha kikao cha kukabiliana na COVID-19

21 Julai 2020

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameitisha kikao maalum cha kilele na magavana siku ya Ijumaa kufuatia ongezeko la visa vya ugonjwa wa COVID-19

https://p.dw.com/p/3fdZP
Kenia Coronavirus  Uhuru Kenyatta Meeting
Picha: PSCU

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Kenyatta amesema kikao hicho kitatathmini utayarifu wa majimbo kukabiliana na virusi hivyo. Taarifa hiyo imesema kuwa, kweye kikao hicho wataangalia mbinu za matibabu ya ugonjwa huo na jinsi ugonjwa huo utakavyokuwa umesambaa katika miezi ya Agosti na Septemba.

Jimbo la Tana River limekuwa jimbo la karibuni zaidi kuripoti kisa cha virusi hivyo na kuongeza idadi ya majimbo yenye visa hivyo kuwa 44 kati ya 47.

Serikali imeonesha wasiwasi wa ongezeko la virusi

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameelezea wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa visa hivyo kila siku. Kenya imerikodi jumla ya visa 13, 770 mapaka sasa, baada ya visa vingine 400 kuripotiwa siku ya Jumatatu. Na katika hatua nyingi soko la maua nchini humo limeanza kupata nuru kwa kiwango cha asilimia 85 katika kipindi hiki ambacho soko la Ulaya linafunguliwa baada ya vizuizi vya kukabiliana na janga la corona.

Soma zaidi: Janga la Covid-19 labisha hodi hospitali kuu ya wazazi Nairobi

Taarifa ya sekta hiyo muhimu ya kibiashara inaonesha Kenya itaingia katika muendelezo kamili wa ufanyaji biashara kwa mwaka ujao. Wakulima wa Kenya walilazimka kuitelekeza shehena ya maua yao baada ya mataifa mengi ya Ulaya kuifunga mipaka yao mwezi Machi na wakazi kuwekewa masharti katika shughuli za mazishi na harusi.