Rais Köhler afanya ziara Afghanistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 21.05.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Rais Köhler afanya ziara Afghanistan

Rais wa Ujerumani Horst Köhler leo amefanya ziara ya ghafla isiyotarajiwa nchini Afghanistan, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Ujerumani kuizuru nchi hiyo katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.

default

Rais wa Ujerumani Horst Köhler

Mara ya mwisho kwa rais wa Ujerumani kuitembelea Afghanistan ilikuwa mwaka 1976 wakati huo rais akiwa Heinrich Lübke.

Rais Köhler akiongozana na mkewe Eva Luise aliwasili katika kambi ya wanajeshi wa Ujerumani kwenye mji wa Mazar-i-Sharif kaskazini mwa Afghanistan. Ziara ya Rais Köhler haikutangazwa kutokana na sababu za kiusalama.Aliwasili akitokea Shanghai China alikotembelea maonesho ya biashara duniani.

Dossier 1 Bundeswehr in Afghanistan

Majeshi ya Ujerumani katika mji wa Masar-i-Scharif kaskazini mwa Afghanistan

Katika ziara yake hiyo Kiongozi huyo wa taifa amewaambia wanajeshi wa Ujerumani kuwa, nchi yao inawaungaa mkono katika jukumu wanazofanya kuisaidia na kuijenga Afghanistan.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com