1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Poland aliyehukumiwa maisha jela Kongo aachiwa huru

28 Mei 2024

Mamlaka nchini Kongo imemuachilia huru raia mmoja wa Poland ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa makosa ya ujasusi.

https://p.dw.com/p/4gO7P
Viongozi wa Kongo wamemuachilia huru raia mmoja wa Poland baada ya kuhukumiwa kifo
Viongozi wa Kongo wamemuachilia huru raia mmoja wa Poland baada ya kuhukumiwa kifoPicha: Arsene Mpiana/AFP/Getty Images

Waziri wa mambo ya nje wa Poland, Radek Sikorski, ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa X kuwa raia huyo, Mariusz Majewski, ameachiliwa. Waziri huyo amechapisha video fupi mtandaoni akionyesha wawili hao wakizungumza kwa njia ya simu.

Hata hivyo, hakutoa maelezo ya sehemu alikokuwa  mtu huyo.

Majewski mwenye umri wa miaka 52 alizuiliwa na wanajeshi wa Kongo mnamo mwezi Februari na kufikishwa mahakamani kwa shutuma za ujasusi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Wiki iliyopita Rais Andrzej Duda alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Kongo, Felix Tshisekedi, juu ya kuachiliwa huru kwa raia huyo wa Poland.