1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJamhuri ya Afrika ya Kati

Raia wa China wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Grace Kabogo
20 Machi 2023

Raia tisa wa China wameuawa baada ya washambuliaji kuuvamia mgodi wa dhahabu kwenye mkoa wa Bambari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

https://p.dw.com/p/4OvnF
Zentralafrikanische Republik Symbolbild Kinder Mine
Picha: Issouf Sanogo/AFP

Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na Meya wa Bambari, Abel Matchipata imeeleza kuwa watu wengine wawili wamejeruhiwa. Meya huyo amesema wahanga ni wafanyakazi wa Kichina katika mgodi wa dhahabu wa Chimbolo, unaoendeshwa na kampuni ya Gold Coast Group.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la waasi linalojulikana kama Muungano wa Wazalendo kwa ajili ya Mabadiliko, CPC ndiyo linashukiwa kuhusika.

Kundi hilo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya majeshi ya serikali. Kundi hilo lina mafungamano na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize.