Polisi Ugiriki wadhibiti mripuko kwenye kifurushi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 05.11.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Polisi Ugiriki wadhibiti mripuko kwenye kifurushi

Kifurushi hicho kilikuwa kimetumwa kwenda katika ubalozi wa Ufaransa uliopo kwenye mji mkuu wa Ugiriki, Athens.

default

Polisi akiwa nje ya ofisi za kampuni ya mizigo mjini Athens, Ugiriki.

Polisi nchini Ugiriki wamefanikiwa kudhibiti mripuko katika kifurushi kilichokuwa na bomu ambacho kilitumwa kwenda katika ubalozi wa Ufaransa mjini Athens.

Pia polisi hao waligundua vifurushi vingine kadhaa walivyokuwa wakivitilia shaka katika kampuni ya mizigo kwenye kitongoji kimoja cha mji huo.

Vifurushi hivyo vimepatikana siku chache baada ya vifurushi vingine vya mabomu kutumwa katika ofisi za balozi kadhaa na viongozi wa Ulaya, akiwemo Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Vifurushi 14 vya mabomu vilipatikana katika wiki iliyopita. Watu wawili wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi lenye msimamo mkali nchini Ugiriki wamekamatwa wakihusishwa na mabomu hayo.

Wakati huo huo, wizara ya ndani nchini Ufaransa imesema kuwa kifurushi kimoja cha bomu ambacho kilizuiliwa nchini Uingereza kikitokea Yemen kwenda Marekani wiki iliyopita, kilikuwa kiripuke dakika 17 tu kabla ya kuzuiwa.

 • Tarehe 05.11.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PzFs
 • Tarehe 05.11.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PzFs

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com