1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya yawatawanya waandamanaji wa upinzani

Grace Kabogo
20 Machi 2023

Polisi nchini Kenya leo wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wa upinzani waliokusanyika nje ya ofisi za serikali katika mji mkuu, Nairobi kwa ajili ya maandamano kupinga mfumuko wa bei.

https://p.dw.com/p/4OvT2
Symbolbild I Polizei in Nairobi
Picha: John Ochieng/SOPA/ZUMA/picture alliance

Waandamanaji pia waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia.

Takribani watu 22 wamekamatwa, wakiwemo wabunge wawili wa upinzani.

Mkuu wa polisi wa Nairobi, Adamson Bungei alisema jana kuwa polisi walipokea maombi ya kufanyika maandamano Jumamosi jioni na mapema Jumapili, ingawa kiutaratibu notisi inatakiwa itolewe siku tatu kabla ya mikutano ya hadhara.

Amesema kwa usalama wa umma polisi haikutoa kibali. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, jana aliwataka Wakenya kujitokeza kwa wingi na kuonesha kutofurahishwa na kile kinachoendelea nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kithure Kindiki alionya jana kuwa yeyote atakayechochea ghasia za umma au kuvuruga amani atachukuliwa hatua.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW
Nenda ukurasa wa mwanzo