1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi 4 wauwa katika shambulizi la wanamgambo Nigeria

5 Aprili 2026

Wanamgambo walivamia jana Jumamosi kituo cha polisi kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuwaua polisi wanne, na pia kulenga kambi ya watu waliokimbia makazi yao.

https://p.dw.com/p/5BgqU
Nigeria Borno 2025 | mauaji
Mauaji yaliofanywa na makundi ya itikadi kali mjini Borno Nigeria, Juni 2025Picha: DW

Polisi inasema magaidi wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram/ISWAP walishambulia makao makuu ya polisi ya tarafa ya Nganzai katika jaribio la kuuteka mji huo, ulioko chini ya umbali wa kilomita 100 kaskazini mwa  Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kundi lingine la wanamgambo wa itikadi kali lililenga lango la kambi inayohifadhi wakimbizi wa ndani huko Damasak, karibu na mpaka na Niger.

Katika taarifa, polisi imesema  washambuliaji hao walimuua afisa wa ulinzi wa kujitolea na kuteketeza takriban nyumba 20 za nyasi.

Imeongeza kuwa katika mashambulizi yote mawili polisi na wakazi waliojitolea walijibu kwa haraka kukabiliana na washambuliaji hao.