Platini ajitumbukiza katika kinyang′anyiro cha urais wa FIFA | Michezo | DW | 31.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Platini ajitumbukiza katika kinyang'anyiro cha urais wa FIFA

Rais wa Shirikisho la Kandanda UIaya – UEFA Michel Platini anatumai kuwa alipiga hatua mwafaka na mapema katika kampeni ya miezi saba ya kuwa rais wa Shirikisho hilo Kandanda la Kimataifa.

Ikiwa bado imesalia miezi mitatu kabla ya kukamilika muda wa mwisho wa kuwasilisha ombi, Platini tayari anaitumia fursa pana kutoka kwa viongozi wa mashirikisho ya kandanda ya mabara sita.

Mfaransa huyo anatumai kuwa na uunwgaji mkono imara kabla ya wagombea wengine kuanza kutoa ushindani wao, na anatarajia kupigia debe na viongozi wa Shirikisho la Kandada barani Asia, (lenye wanachama 46 wa FIFA watakaopiga kura) na CONMEBOL (wanachama 10).

Hata hivyo Asia ni nyumbani kwa mgombea mpinzani tajiri mkubwa wa Korea kusini Chung Mong-joon ambaye amethibitisha anajiunga na kinyang'anyiro hicho.

Chung Mong-joon amemueleza mtu anayepigiwa upatu kuchukua wadhifa huo Michel Platini kuwa ni kibaraka asiyeaminika ambaye anahusika na kashfa. Chung ambaye ni makamu wa zamani wa rais wa FIFA amejieleza kuwa ni mgombea asiyehusika na rushwa akiwa na mtazamo wa kidunia badala ya bara la Ulaya na kulipeleka shirika hilo la kandanda duniani katika enzi mpya.

Tajiri huyo kutoka familia inayomiliki kampuni kubwa la Hyundai amesema atatangaza nia yake hiyo wiki ijayo na pia ameahidi kwamba iwapo atachaguliwa , atatumikia kipindi kimoja tu cha miaka minne.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef