1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PEKING:Kimbunga "Krosa chaikumba China"

7 Oktoba 2007

Kimbunga kikali ambacho tayari kimesababisha madhara nchini Taiwan leo kimeikumba China kikiwa na mwendo wa kilometa zaidi ya mia moja kwa saa.

https://p.dw.com/p/C781

Kimbunga hicho kimezikumba sehemu za mashariki mwa China baada ya Mamilioni ya watu kuhamishiwa kwenye sehemu za usalama .

Kimbunga hicho kinachoitwa Krosa kiliuwa watu watano nchini Taiwan.Maafisa wa China wamesema dhoruba hiyo illifikia mwendo wa kilometa 126 kwa sasa.Lakini hakuna habari iwapo kimesababisha madhara nchini China vilevile.