Papa Francis asifiwa kwa uteuzi wa makadinali wapya | Masuala ya Jamii | DW | 05.01.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Papa Francis asifiwa kwa uteuzi wa makadinali wapya

Uteuzi mpya wa makadinali wa Kanisa Katoliki uliotangazwa na Mkuu wa Kanisa hilo, Papa Francis, hapo jana umepongezwa na jamii ya kanisa, kwani sehemu kubwa ya wateule hao ni kutoka Asia, Amerika Kusini na Afrika.

Papa Francis akisalimiana na makadinali kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Papa Francis akisalimiana na makadinali kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Dk. Charles Kitima, mtaalamu wa Sheria za Kanisa na Sheria za Kimataifa, ambaye pia ni mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Mtakatifu Augustine, Mwanza, Tanzania, anasema uteuzi huu mpya unamaanisha kwamba Papa Francis anataka Kanisa Katoliki liwe karibu zaidi na wafuasi wake hata kama wanatokea kwenye mataifa machanga na masikini.

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Iddi Ssessanga

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com