Pakistan yafanya maandalizi ya mazungumzo ya amani
20 Aprili 2026
Matangazo
Rais wa Marekani Donald Trump amesema wapatanishi wa Marekani wataelekea Pakistani leo, lakini haijabainika wazi kama mipango hiyo itabadilika.
Kwa upande wake, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Esmail Baghaei, amewaambia waandishi wa habari mjini Tehran leo kwamba hakuna maamuzi yaliofikiwa kuhusu mazungumzo hayo.
"Kwa sasa, nikiwa nahudumu, hatuna mipango ya awamu inayofuata ya mazungumzo, na hakuna uamuzi wowote uliotolewa kuhusu hili."
Huku hayo yakijiri, China imeelezea leo wasiwasi kuhusu hatua ya Marekani ya kukamata meli yenye bendera ya Iran iliyojaribu kukwepa kizuizi cha majini, na kuzitaka pande zote mbili kurejelea mazungumzo ya amani.