1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan kuwafurusha wahamiaji mwezi ujao

Sudi Mnette
4 Oktoba 2023

Serikali ya Pakistan imetangaza kufanya operesheni kubwa ya kuwafurusha wahamiaji walioingia nchini humo kinyume, ikiwa tahadhari kwa wakazi wasio na hati za makazi wakijumuishwa Waafghanstan takriban milioni 1.7.

https://p.dw.com/p/4X5Ab
Waziristan, Pakistan
Picha: Faridullah Khan/DW

Waziri wa Mambo ya Ndani wa taifa hilo Sarfraz Bugti amesema operesheni hiyo haitowalenga Waafghanistan pekee na kwamba itawahusu pia watu wa mataifa yote, ingawa idadi kubwa ya wakazi hao wageni ni raia wa taifa hilo.

Bugti amesema kuwa wahamiaji wowote nchini Pakistan wanaoishi kinyume cha sheria wanapaswa kwenda makwao kwa hiari kabla ya mwishoni mwa Oktoba ili kujiepusha na kurejeshwa kwa lazima.

Kampeni hiyo inatangazwa wakati kukiwa na uhusiano mbaya kati ya Pakistan na taifa jirani yake Afghanistan kwa kile Pakistan inakisema kuwa serikali ya taifa hilo inafadhili makundi ya wanamgambo ambao wanaingia katika ardhi yao na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kisha kwenda kupata hifadhi Afghanistan.