Osaka na Thiem mabingwa wa China Open | Michezo | DW | 07.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Osaka na Thiem mabingwa wa China Open

Kulikuwa na fainali ya China Open ambapo majina yote makubwa katika Tennis yalikuwa huko Beijing kuchuana ambapo mabingwa hatimaye walibainika baada ya mchuano mkali mno. Lakini wawili tu ndio walioondoka na mataji.

Mchezaji nambari nne duniani upande wa kina dada Naomi Osaka alikuwa na wakati mgumu dhidi ya Ash Barty ambaye ndiye mchezaji nambari moja ila hatimaye alipata ushindi wa seti tatu za 3-6 6-3 6-2 na kunyakua taji lake la pili baada ya kushinda lile la Pan Pacific Open nchini Japan mwezi uliopita.

Bingwa wa kina kaka alikuwa Dominic Thiem kutoka Austria alimbwaga Stefanos Tsitsipas kutoka Ugiriki kwa serti tatu za 3-6 6-4 6-1. Huyu hapa Thiem baada ya ushindi huo.

"Kwa kweli nafikiri ilikuwa mojawapo ya mechi nzuri zaidi nilizowahi kucheza na siku na makosa mengi. Mwanzoni nilikuwa na wakati mgumu kwasababu Stefanos aliipeleka mechi kwa kasi sana. Lakini baadae nilikua nilijikaza hasa katika seti ya pili na ya attu na sifikiri kama naweza kucheza vyema zaidi ya vile. Kwa hiyo ilikuwa wiki njema kwangu," alisema Thiem.