Operesheni ya pamoja ya DRC na Uganda yamaanisha nini? | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 30.11.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Operesheni ya pamoja ya DRC na Uganda yamaanisha nini?

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zilianza hapo jana oparesheni ya pamoja ya angani mashariki mwa Congo dhidi ya waasi wa ADF. Babu Abdallah amezungumza na mchambuzi wa masuala ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye ameanza kwa kutoa tathmini yake juu ya oparesheni hiyo ya kijeshi?

Sikiliza sauti 03:06

Msemaji wa jeshi la Uganda Flavia Byekwaso alithibitisha kutokea kwa shambulio hilo la anga kupitia mtandao wake wa Twitter bila ya kutoa maelezo zaidi. Hata hivyo Jumatatu wiki hii serikali ya Congo ilikanusha kwamba ilikubaliana kufanya oparesheni ya pamoja na Uganda.