Operesheni ya kijeshi yaanza katika mji wa Slovyansk | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Operesheni ya kijeshi yaanza katika mji wa Slovyansk

Jeshi la Ukraine linaripotiwa kuanza operesheni ya kijeshi kuudhibiti mji wa Mashariki mwa Ukraine wa Slovyansk.Kuna taarifa kuwa helikopta moja imedunguliwa katika mji huo

Shirika la habari la Ujerumani Dpa limeripoti kuwa helikopta mbili za kijeshi zimedunguliwa na rubani mmoja ameuawa huku mwingine akitekwa nyara.Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine na kujiunga na Urusi wamesema wanajeshi hao wameanzisha kile walichokiita operesheni kubwa katika mji wa Slovyansk.Milio ya risasi na miripuko imesikika viungani mwa mji huo.Serikali ya Ukraine haijazungumzia operesheni hiyo ya kijeshi iliyoanza muda mfupi uliopita.Mengi zaidi kuhusu hali inavyojiri mashariki mwa Ukraine ni hivi punde.

Mwandishi:Caro Robi/dpa/Dw English

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com