1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ongezeko la maambukizi ya Corona latia hofu Ujerumani

Sekione Kitojo
8 Oktoba 2020

Ujerumani inapitia katika kipindi kinachotia hofu baada ya kupanda kesi za maambukizi ya virusi vya corona, waziri wa afya Jens Spahn amesema, huku maambukizi mapya ya kila siku yakiongezeka kupita 4,000 tangu Aprili.

https://p.dw.com/p/3jcJG
Berlin | Pressekonferenz zu Pflege und Corona: Jens Spahn
Jens Spahn , waziri wa afya wa UjerumaniPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture-alliance

Lothar Wieler, mkuu  wa  taasisi ya  udhibiti  wa  magonjwa ya  Robert Koch , ameonya  kwamba  Ujerumani  inaweza kushuhudia  usambaaji  ambao  hautaweza  kudhibitiwa wa  virusi  vya  corona. Nchi  hiyo  yenye  uchumi  mkubwa barani Ulaya  ilirekodi  maambukizo  mapya  ya  COVID-19 , 4,058 katika  muda  wa  masaa  24, ikiwa  ni  ongezeko kubwa  katika  idadi  iliyotolewa  jana  ya  watu 2,828, kwa mujibu wa  Taasisi  ya  Robert Koch.
 

Berlin | Pressekonferenz 100 Tage Corona-Warn-App, 23.09.2020  Jens Spahn
Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn (katikati) akizungumza na waandishi habariPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture-alliance

"Tarakimu  hizo zinaonesha  ongezeko linalotia  hofu ," Spahn  waziri  wa  afya  wa  Ujerumani  aliwaambia waandishi  habari  mjini  Berlin, na  kuwataka  Wajerumani kutopuuzia hatua  za  kuzuwia  usambaaji  wa  virusi  hivyo hatari.


"Hakuna nchi nyingi  barani Ulaya ambazo zimeweza kupambana  na  mzozo  huo pia  hadi sasa,"  amesema. "Lakini  hatuwezi  kuchukulia  kama  mchezo wa  kamari kile  ambacho  tumefanikiwa  hadi sasa."
 

Ongezeko hilo la maambukizo  linalotia  hofu  limekuja wakati  wa  likizo za shule  katika  majira  haya  ya mapukutiko zikianza   ama  zikiendelea  nchini  Ujerumani, na  kusababisha  miito  kutoka  katika  serikali  ya  kansela Angela  Merkel  kwa  raia  kuepuka  kusafiri  nje  ya  nchi wakati  huu  wa  kipindi  chenye  shughuli  nyingi  kwa  ajili ya  utalii.

Berlin | Angela Merkel bei Verleihung des Integrationspreises
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: Kay Nietfeld/Reuters

Majimbo yaimarisha sheria kuhusu virusi vya corona
 

Majimbo 16 ya  Ujerumani  pia yameimarisha  sheria kwa ajili  ya  safari  za  ndani, ambapo wengi  wakikubaliana  na marufuku ya  kukaa  katika  mahoteli, ama  nyumba za kukodi wakati  wa  likizo kwa  wasafiri  kutoka  katika maeneo  yanayofahamika  kama  yenye  hatari  nchini humo.
 

Serikali  ya  Uingereza  inatafakari  kuweka  vizuwizi  vipya katika  maisha  ya  kila  siku  nchini  Uingereza  huku kukiwa  na  ushahidi  kuwa  hatua  hadi  sasa  hazijaleta mafanikio  ya  kutosha  kuzuwia  maambukizi  mapya  ya virusi  vya  corona. Wakati  idadi  ya  watu  wanaohitaji kwenda  hospitali  wakiwa  na  dalili  zinazoelekea  kuwa na maambukizo   ya  virusi  vya  corona  ikiongezeka,  na katika  baadhi  ya  maeneo  kaskazini  mwa  Uingereza  hali ikiwa  ni  mbaya, shinikizo dhidi  ya  serikali  kuchukua hatua  zaidi  linaongezeka pia.

Großbritannien, London | Boris Johnson im Parlament
Waziri mkuu wa Uingereza Boris JohnsonPicha: PRU/AFP

Kampuni  ya  Gilead Sciences  imesema  leo kuwa imekubali  kuiuzia ulaya  hadi  dozi 500,000 la  dawa  ya remdesivir, wakati  bara  la  Ulaya  linahangaika  kuongeza upatikanaji wa  dawa  hiyo  ambayo  ni moja  kati  ya  dawa aina  mbili  zilizothibitishwa  hadi  sasa  kutibu wagonjwa wa  COVID-19. Makubaliano  hayo  yanajumuisha  ununuzi wa  dawa hiyo  kwa  miezi  sita  ijayo kwa  mataifa  27 wanachama  wa  Umoja  wa  Ulaya , Uingereza, mataifa sita  ya  eneo  la  balkan pamoja  na  Iceland, Liechtenstein na  Norway.