1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Norway yaisihi China iilete Urusi izungumzie amani Ukraine

Josephat Charo
7 Julai 2026

Norway imeitaka China isaidie kuileta Urusi kwenye meza ya mazungumzo ya amani ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/5GgTp
Waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere ameitaka China iishawishi Urusi ikae katika meza ya mazungumzo ya amani ya Ukraine.
Waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere ameitaka China iishawishi Urusi ikae katika meza ya mazungumzo ya amani ya Ukraine.Picha: Christophe Petit Tesson/AP Photo/picture alliance

Norway inaihimiza China itumie uhusiano wake wa karibu na uongozi wa Urusi kusaidia kuleta suluhu ya mazungumzo kwa vita nchini Ukraine na pia kwa ajili ya uhusiano bora na Ulaya.

Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere Jumatatu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi huko mjini Oslo.

Stoere alisema sehemu kubwa zaidi ya majadiliano yao ilijikita katika suala la Ukraine.

Wang alikuwa ziarani Norway baada ya kuzitembelea Denmark, Sweden na Finland.