1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini kurejesha hatua za kijeshi dhidi ya Kusini

23 Novemba 2023

Korea Kaskazini imesema itarejesha hatua zote za kijeshi ilizokuwa imeziondoa chini ya mpango wa 2018 na Korea Kusini uliodhamiria kupunguza mvutano kwenye mpaka wao wa pamoja, ikiapa kupeleka vikos na silaha mpya.

https://p.dw.com/p/4ZLDR
Südkorea | TV-Übertragung Nordkorea | 75. Gründungstag der Arbeiterpartei
Picha: Jung Yeon-Je/AFP/Getty Images

Tangazo hilo la wizara ya ulinzi ya Korea Kaskazini limejiri siku moja baada ya Korea Kusini kusitisha sehemu ya makubaliano ya Korea zote mbili kama jibu la hatua ya Pyongyang kurusha angani satelaiti ya ujasusi na kusema itaimarisha maramoja ufuatiliaji kwenye mpaka wenye ulinzi mkali na Korea Kaskazini. Korea Kaskazini imeituhumu Korea Kusini kwa kuufuta mpango huo, unaofahamika kama Mkataba Kamili wa Kijeshi, na kusema Seoul itawajibishwa ikiwa kutatokea mgongano usioweza kurekebeshika kati ya Korea hizo mbili.