Nigeria yazungumza na Boko Haram | Matukio ya Afrika | DW | 23.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Nigeria yazungumza na Boko Haram

Mamlaka nchini Nigeria zinaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo yanayolenga kuwaokoa baadhi ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na kundi la Boko Haram mwaka 2014, katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.

Msemaji wa rais wa Nigeria,  Garba Shehu, amesema kwenye mtandao wa Twitter, kwamba majadiliano yanayoendeshwa chini ya Wizara ya Usalama yanaleta matumaini makubwa ya kufanikiwa.

Alikuwa akizungumzia taarifa kwamba, tayari kuna wasichana waliokwishaachiliwa hivi karibuni, akisema kuwa bado hilo halijafanyika, ingawa litawezekana.

Kiasi cha wasichana 270 walitekwa mwezi Aprili 2014 kutoka skuli yao mjini Chibok, jimbo la Borno, ambako Boko Haram wanaendesha vita kwa mwaka wa saba sasa.

Watu 15,000 wameshauawa kwenye vita hivyo, ambavyo pia vimewasababishia wengine zaidi milioni mbili kukimbia makaazi yao.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com