Nigeria: Watu 15 wauwawa na Boko Haram | Matukio ya Afrika | DW | 01.11.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Nigeria: Watu 15 wauwawa na Boko Haram

Washukiwa wa kundi la Boko Haram wamewaua watu 15 kaskazini mashariki mwa Nigeria

Picha ya maktaba

Picha ya maktaba

Watu wanaoshukiwa  kuwa  wanachama  wa  kundi   la Kiislamu  la  Boko Haram  wamewauwa  kiasi  watu 15 katika  shambulio  dhidi  ya  vijiji  kaskazini  mashariki  mwa Nigeria  jioni  ya  Jumatano, wakaazi  wa  eneo  hilo wameliambia  shirika  la  habari  la  Reuters. 

Vijiji  hivyo  viko  nje  kidogo  ya  mji  wa  Maiduguri, kaskazini  mashariki  mwa  nchi  hiyo  na  makao  makuu ya  juhudi  za  kupambana  na  kundi  la  Boko  Haram pamoja  na  wapiganaji  wengine  wanaohusika  na  kundi hilo  katika  mataifa  ya  Afrika  magharibi.

Mzozo  huo  umekuwapo  katika  eneo  hilo  kwa  karibu miongo  kadhaa. Licha  ya  taarifa  hiyo  ya  serikali  ya Nigeria  tangu mwishoni  mwa  2015  kwamba  Boko Haram kwa  kiasi  kikubwa  imeshindwa, wapiganaji  hao  bado wana  uwezo  wa  kushambulia ndani  na  kuzunguka mji wa  Maiduguri  na  sehemu  nyingine  kubwa  za  eneo  hilo la  kaskazini  mashariki.