1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria na Ghana zashindana kuanzisha sarafu za kidijitali

Grace Kabogo
22 Septemba 2021

Nigeria na Ghana zashindana juu ya kuanzisha sarafu ya kidijitali katika benki kuu, wakati ambapo zikiangalia umaarufu wa wimbi la kuwekeza katika sarafu za kidijitali likishika kasi kwenye mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/40eCd
Symbolbild Dogecoin
Picha: STRF/STAR MAX/IPx/picture alliance

Benki kuu za nchi hizo mbili zinashirikiana na kampuni za kifedha za kigeni kuanzisha sarafu zao za kidijitali, na kujiunga na nchi zinatotumia mfumo huo.

Nigeria itazindua sarafu yake ya kidijitali ya eNaira Oktoba Mosi, huku Ghana nayo ikiaanza majaribio ya kuzindua sarafau yake ya e-Cedi mwezi huu.

Nigeria imeshuhudia kuongezeka wa uwekezaji katika sarafu za kidijitali, licha ya marufuku ya kuuza na kununua sarafu za kidijitali iliyowekwa na mabenki.

Wanigeria wanaingia kwenye biashara hiyo kutokana na kushuka thamani ya sarafu ya Naira na kukabiliana na gharama kubwa za maisha pamoja na ukosefu wa ajira.

Benki kuu ulimwnguni kote zinatafuza njia za kuanzisha sarafu za kidijitali zitakazotumika kwa malipo halali kutokana na kuongezeka kwa miamala ya kielektroniki na sarafu za kidijitali.