NEW YORK: Mwanamfalme Charles atunzwa | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Mwanamfalme Charles atunzwa

Aliyekuwa makamu wa rais nchini Marekani, Al Gore, amemkabidhi mwanamfalme Charles wa Uingereza zawadi kwa kazi yake ya kuyalinda mazingira.

Al Gore, aliyefanya kazi wakati wa utawala wa rais Bill Clinton katika miaka 1990, alimpa zawadi hiyo mwanamfalme Charles inayotolewa na taasisi ya afya na mazingira katika chuo kikuu cha Havard, wakati Charles na mkewe Camilla walipokuwa wakikamilisha ziara yao ya siku tatu nchini Marekani.

Ziara yao ililenga maswala yanayohusu maendeleo ya vijana, ukarabati wa maeneo ya mijini na maongozi bora katika maswala ya mazingira.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com