Neuer ndiye mlinda lango bora | Michezo | DW | 14.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Neuer ndiye mlinda lango bora

Nani mwingine ambaye FIFA ingemchagua kuwa mlinda lango bora zaidi katika Kombe la Dunia? Hata katika dimba lililojaa wagombea wengi, Manuel Neuer wa Ujerumani aliibuka kileleni.

Hii ni kutokana na ustadi wake wa kupangua makombora na pia kucheza nje ya kijisanduku chake. Huenda Algeria ingeipiku Ujerumani bila Manuel Neuer ndani ya lango? Bila ya shaka, Wajerumani wangefungwa goli la mapema na Islam Slimani, kama Neuer hangekabiliana na mshambuliaji huyo nje ya kijisanduku chake na kuuondoa mpira.

Akizungumza baada ya fainali, Neuer alisema: “Sijui tutasheherekea hadi saa ngapi, lakini najua tutaamka na maruweruwe. Tumefanya kazi pamoja vizuri tangu tulipoanza maandalizi yetu, wakati tulipopata pigo la kuwapoteza wachezaji kama vile kaka wawili Sven na Lars Bender na Marco Reus. Lakini wao ni mabingwa wa Ulimwengu pia. Wajerumani wote ni mabingwa wa Ulimwengu“.

Kombe la Dunia 2014 limekuwa na wagombea wakuvutia wa Tuzo ya Glovu ya Dhahabu (mlinda lango bora) kutoka kwa “waziri wa ulinzi wa siku za usoni wa Marekani” Tim Howard, hadi kwa Guillermo Ochoa wa Mexico au Keylor Navas wa Costa Rica.

Nguvu mpya Tim Krul alijitengenezea jina katika mikwaju ya penalti, huku Sergio Romero wa Argentina akiinyima Uholanzi nafasi kwa kuzuia penalti. Lakini Neuer, ambaye hakuwahi kukumbana na penalti akiwa na Ujerumani, ndiye aliyeng'ara zaidi katika kundi hili. Katika dakika 420 za mchezo katika hatua ya mchujo, kipa huyo wa Ujerumani alikubali kufungwa magoli mawili pekee.

Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: Iddi Sessanga