1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benjamin Netanyahu aidhinisha operesheni ya Rafah

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameidhinisha mipango ya operesheni ya kijeshi katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah.

https://p.dw.com/p/4dgA3
Israel | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abir Sultan/AP/dpa/picture alliance

Taarifa iliyotolewa na ofisi yake imeeleza kwamba sambamba na mipango ya kuwapeleka wanajeshi, lakini pia jeshi linajiandaa kwa ajili ya kuwahamisha raia. 

Hatua hiyo imechukuliwa licha ya kuongezeka ukosoaji wa kimataifa kuhusu uwezekano wa operesheni ya Rafah. Zaidi ya Wapalestina milioni moja wanajihifadhi karibu na mji huo, baada ya kukimbia mapigano katika maeneo mengine ya Ukanda wa Gaza.

Israel yatuhumiwa kuwaua watu 20 waliokuwa wakisubiri msaada

Netanyahu pia amerejelea tathmini yake kwamba pendekezo la Hamas la kusitisha vita huko Gaza halina mashiko. Hayo yanajiri mnamo wakati ujumbe wa Israel ukielekea Doha mara baada ya mkutano wa baraza la usalama la Israel kuhusu msimamo wa nchi hiyo.