1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

NATO yatoa wito kwa Urusi kuheshimu anga la Poland

10 Septemba 2025

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema kitendo cha Poland kuzidungua droni za Urusi zilizoingia kwenye anga ya nchi hiyo mapema hii leo kimeonyesha wazi kwamba Ulaya inaweza kujilinda yenyewe.

https://p.dw.com/p/50IbE
Poland I Donald Tusk
Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk akiwa katika kikao na maafisa wa serikali na wakuu wa kijeshi kujadili droni za UrusiPicha: Chancellery of the Prime Minister of Poland via AP/picture alliance

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema kitendo cha Poland kuzidungua droni za Urusi zilizoingia kwenye anga ya nchi hiyo mapema Jumatano kimeonyesha wazi kwamba Ulaya inaweza kujilinda yenyewe lakini inapaswa kujiimarisha zaidi.

Poland ilizidungua droni za Urusi zilizolengwa kwenda kuyashambulia maeneo ya magharibi mwa Ukraine ambayo yanapakana na Poland.

Hatua hiyo ilipelekea kufanyika kwa mkutano wa baraza la Jumuiya ya Kujihami ya NATO mapema Jumatano na kufanya tathmini ambayo mkuu wa muungano huo Mark Rutte amesema ni hatua ya hatari na kwamba Vladmir Putin lazima aheshimu anga la taifa jingine na kwamba kama NATO.

Urusi yenyewe kwa upande wake imegoma kutoa maoni juu ya sakata hilo. Alipoulizwa na waandishi wa habari Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwajibu kwamba wizara ya ulinzi itafutwe na kutoa majibu ya suala hilo.