Mwingine atupwa nje kinyanganyiro cha urais Misri | Matukio ya Afrika | DW | 24.04.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mwingine atupwa nje kinyanganyiro cha urais Misri

Tume ya uchaguzi nchini Misri imemzuia kugombea urais, aliyekuwa Waziri Mkuu wa katika siku za mwisho za utawala wa rais Hosni Mubarak Ahmed Shafiq na hivyo kumuacha Amr Moussa kupambana na wanaharakati wa kiislam.

Khairat al-Shater

Khairat al-Shater

Hatua hii imefuata kuidhinishwa kwa sheria inayowazuia maafisa wote waliohudumu chini ya utawala wa rais Hosni Mubarak kugombea urais nchini humo na Baraza la utawala wa kijeshi siku ya jumanne.

Kuondolewa kwa Ahmed kunaamanisha kuwa Misri sasa itaongozwa na rais asiye na historia ya jeshi kwa mara ya kwanza tangu wanajeshi walipoupindua utawala wa kifalme mwaka 1952. Shafiki alikuwa kamanda wa vikosi vya anga vya Misri na kwa baadhi alikuwa anaonekana kama chaguo la wanajeshi tangu alipotangaza nia yake ya kuogombea.

Kuondolewa kwake pia kunapunguza nafasi za wapiga kura wasiopenda kuwa na rais ambaye ni mwanaharakati wa kiislam. Wagombea wanaopewa nafasi kubwa zaidi kwa sasa ni Mohamed Mursi anaeungwa mkono na chama cha Udugu wa Kiislam (Islamic Brotherhoo), na Abdel Moneim Abol Fatouh, mwanachama wa zamani wa chama hicho aliyesema ana uhakika wa kushinda wakati akizungumza na shirika la habari la Reuters siku ya Jumanne.

Misri itafanya uchaguzi wa kwanza wa rais tangu kuondolewa kwa Hosni Mubarak tarehe 23 na 24 Mei, ikiwa ni hatua ya mwisho kabla majenerali wa kijeshi kukabidhi mamlaka kwa rais wa kiraia Julai mosi mwaka huu.

Kwa sasa, maoni yanaonyesha kuwa Amr Moussa ataingia katika duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mmoja wa wanaharakati wa kiislam lakini wapiga kura wengi bado hawajaamua nani watakayemchagua. Mustafa Kamel, Profesa wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Cairo alisema Moussa anaweza kupata za wale waliokuwa wamepanga kumchagua Shafiq.

Ahmad Shafiq

Ahmad Shafiq

Mgogoro juu ya nani anapaswa kugombea nafasi hii umezua upinzani kutoka kwa wafuasi wa wagombea wawili kutoka vyama vya kiislam ambao walipigwa marufuku katika hali iliyotia doa mchakato wa Misri kuelekea katika demokrasia ya kweli, ambapo pia makamu wa rais wa zamani wa Hosni Mubarak naye alizuiwa kugombea katika uchaguzi huu.

Muongozo huu, ambao ni marekebisho ya sheria ya haki za kisiasa, unawahusu wote waliyowahi kuhudumia katika nafasi za juu serikalini na chini ya chama tawala wakati wa muongo wa mwisho wa utawala wa rais Hosni Mubarak.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga\RTRE
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman